FAHAMU FAIDA ZA BAMIA

Watu wengi hudhani kuwa ulaji wa bamia ni kwa kundi la watu wa hali ya chini sana la hasha ziko nyingi za matumizi ya bamia kwa afya ya mwanadamu. Mojawapo ya faida ambayo ni muhimu ni kusaidia kumeng’enya sukari mwili au kuweka sawa mfumo wa sukari mwilini na pia tatizo la kukosa choo ni tatizo la kawaida kwa wagonjwa wa Kisukari. Bamia ikiliwa mara kwa mara inasaidia kurekebisha mfumo wa umeng’enya chakula na sukari mwilini. Angalizo kwa wagonjwa wa kisukari, msiache dawa zenu na kuanza kutumia bamia kama dawa. Majimaji yanayotoka katika bamia yana uwezo wa kuondoa lehemu katika mishipa ya damu kwenye mwili. Tumia bamia mara kwa mara kama tunda mboga linalosaidia kumeng’enya sukari mwilini na kuimarisha kinga ya mwili wako. Tukiachana na kisukari, bamia huongeza na huboresha kinga ya mwili hasa kwa watu ambao kinga yao ya mwili imeshuka kama vile watu wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU). Wataalamu lishe wanasema watu wengi wamekuwa wakila bamia kwa kuidharau ila huzuia magonjwa ya moyo kwa kuisaidia mishipa ya damu kufanya kazi vizuri. Watu wenye matatizo ya vidonda vya tumbo, bamia huwasaidia kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tumbo na huongeza kiwango cha damu mwilini. Wengine wanatumia bamia kama dawa ya kuongeza kinga ya mwili kwa kutafuna zikiwa mbichi au kuzichemsha. Faida nyingine ya ulaji wa bamia ni kuusaidia mwili kusafisha damu. Ulaji wa bamia husaidia kutibu tatizo la upungufu wa damu. Bamia pia huondoa sumu mwilini na faida nyingine ni kuimarisha mifupa pamoja na mfumo wa uonaji kwa sababu ina chanzo kizuri cha vitamin A na Beta carotene.

Comments

Popular Posts